• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NASA yatangaza sehemu tatu ambazo moja itachaguliwa kuwa mahali pa kutua chombo cha uchunguzi wa Mars

  (GMT+08:00) 2017-02-15 19:50:52

  Idara ya safari za anga za juu ya Marekani NASA imetangaza sehemu tatu kwenye sayari ya Mars ambazo moja itachaguliwa kuwa mahali pa kutua chombo kipya cha uchunguzi wa sayari hiyo kiitwacho "Mars 2020".

  Sehemu hizi tatu ni pamoja na eneo la NE Syrtis, shimo la Jezero na mlima Columbia. Wanasayansi wanaridhika zaidi na shimo la Jezero, ambalo liliwahi kuwa ziwa.

  Kwa mujibu wa mpango, chombo cha "Mars 2020" kitarushwa angani kwa roketi ya AtlasV mwezi Julai au Agosti mwaka 2020 kutoka jukwaa la kurushia roketi la No. 41 la kituo cha jeshi la anga la Cape Canaveral jimboni Florida, Marekani. Chombo hiki kitachunguza hali ya kijiografia kando ya mahali pa kutua, kutafiti kama mazingira ya huko yanafaa kwa maisha ya viumbe au la, kutafuta dalili ya kuwepo kwa viumbe katika zama za kale, kuchambua rasilimali zitakazogunduliwa na wanaanga na tishio kwa wanaanga.

  Chombo hiki kitakusanya sampuli hizo kwa miaka miwili, lakini hakitarudi duniani. Sampuli huenda zitapelekwa duniani kupitia jukumu lifuatalo la uchunguzi wa sayari ya Mars.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako