• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Japan yasanifu mfumo wa kukodi betri za baiskeli barabarani

  (GMT+08:00) 2017-02-16 16:33:31

  Kampuni ya Panasonic hivi karibuni imeonesha teknolojia mbalimbali mpya zinazosaidia kuboresha maisha ya mijini, zikiwemo teknolojia ya video zenye upana wa piseli elfu 8, roboti inayotoa huduma kwenye uwanja wa ndege, chombo cha kutafsiri kwa lugha nyingi na mfumo wa kukodi betri za baiskeli barabarani.

  Wakazi wengi mjini Tokyo wanapanda baiskeli zenye giaboksi au betri. Wale wanaopanda baiskeli zenye betri husumbuliwa na kuisha kwa betri njiani, hivyo wanahitaji kuzichaji mara kwa mara.

  Kampuni ya Panasonic na kampuni ya Docomo zimeshirikiana kusanifu mfumo wa kukodi betri za baiskeli barabarani. Masanduku yenye betri iliyochajiwa yatawekwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo maduka madogomadogo, na wateja wataweza kubadilisha betri za baiskeli zao wenyewe na kulipa kwa kadi au simu za mkononi.

  Licha ya betri, kampuni ya Panasonic pia imetoa huduma ya kukodi betri za baiskeli barabarani. Mwaka jana kampuni hiyo imefanya majaribio mjini Tokyo, inasema inatarajia mfumo huo utatumiwa rasmi kwa kutumia fursa ya michezo ya Olimpiki ya Tokyo itakayofanyika mwaka 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako