• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Sudan yazidi laki 3

  (GMT+08:00) 2017-02-18 19:19:38
  Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu OCHA nchini Sudan imesema hivi sasa idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Sudan imezidi laki 3.

  Taarifa iliyotolewa na Ofisi hiyo imesema, wakimbizi wa Sudan Kusini walianza kukimbia nchini Sudan baada ya kutokea mapambano ya kijeshi nchini Sudan Kusini mwezi Decemba mwaka 2013. Kutokana na hali ya wasiwasi nchini Sudan Kusini na ukosefu wa chakula, wakimbizi wengi wa Sudan Kusini waliendelea kuingia nchini Sudan kuanzia mwezi Januari mwaka jana, na kwamba wengi wa wakimbizi hao wametoka jimbo la North Bahr el Ghazal na jimbo la Warab.

  Taarifa hiyo imesema, asilimia 65 ya wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Sudan ni watoto, ambao wengi walikuwa na tatizo la utapiamlo. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaandaa mpango wa usimamizi wa raslimali ili kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi hao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako