• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya China yatoa ripoti kuhusu kutekeleza sera imara za sarafu

    (GMT+08:00) 2017-02-20 21:12:54

    Hivi karibuni Benki ya umma ya China imetoa ripoti kuhusu utekelezaji wa sera za sarafu za China kwa robo ya nne ya mwaka 2016, ikisema kuwa katika kipindi kijacho, China itatekeleza sera imara ya sarafu, kuongeza ufanisi wa hatua za udhibiti na marekebisho, ili kutoa mazingira mazuri kwa ajili ya mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa. --- ana maelezo zaidiā€¦

    Ripoti hiyo imeeleza kuwa, tokea mwaka 2016 mzunguko wa mfumo wa benki ni mzuri, huku utoaji wa mikopo na uchangishaji wa fedha katika jamii ukiongezeka kwa hatua madhubuti na kwa kasi, wakati huo huo kiwango cha riba kiko chini.

    Benki kuu ya China ikizungumzia sera za sarafu katika kipindi kijacho inasisitiza kuwa itaendelea kufuata kanuni ya kupata maendeleo kwa hatua madhubuti, na kuweka mazingira mazuri ya fedha kwa ajili ya mageuzi ya kimuundo. Wachambuzi wameeleza kuwa, hatua hiyo imeonesha kuwa sera ya sarafu ya China imebadilika. Mtafiti mwandamizi wa Benki ya China Bw. Zong Liang anasema:

    "Sera hiyo inahimiza kupandishwa kwa kiwango cha riba ya sarafu ya China RMB, hali ambayo inasaidia kupunguza shinikizo la mzunguko wa fedha za kimataifa."

    Naibu mkurugenzi wa Benki kuu ya China Bw. Yi Gang akizungumzia mwelekeo huo wa sera ya sarafu anasema, benki hiyo itaendelea kutekeleza sera ya hatua madhubuti ya fedha, si ya kubana wala ya kulegeza. Mchumi mwandamizi wa Benki ya CITIC Bw. Chu Jianfang pia amesema, ingawa sera ya sarafu imebadilika, lakini haijafikia kiwango cha kubana matumizi ya fedha, wala haijaingia katika njia ya kuongeza kiwango cha riba.

    Aidha ripoti hiyo ya sera ya sarafu imezingatia kuboresha muundo wa kuhimiza mzunguko wa sarafu, hatua ambayo italeta athari kwa mzunguko wa utoaji wa mikopo inayofuatiliwa na watu. Mtafiti mwandamizi wa Benki ya China Bw. Zong Liang anasema:

    "Utoaji wa mikopo katika mwezi wa Januari ulikuwa ni mkubwa zaidi, hivyo tunataka kuonesha ishara ya kubana matumizi ya sarafu, na kuiweka katika kiwango mwafaka. Pili, kati ya utoaji wa mikopo ya aina mbalimbali, mikopo mingi zaidi inahusu mali zisizohamishika, serikali na kampuni kubwa. Tunatumai muundo wa utoaji wa mikopo utazidi kuboreshwa, ili kuelekeza mikopo kutumiwa katika viwanda vidogo na vyenye ukubwa wa kati."

    Mbali na hayo, ripoti hiyo pia inasisitiza kudhibiti na kuzuia hatari za fedha, na kufuatilia kwa makini bei za vitu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako