• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongeza nguvu katika kuvutia fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2017-02-21 17:50:39

    Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng amesema, kauli kuhusu kuondoa uwekezaji kutoka China si ya kweli, kwani kuvutia fedha za kigeni ni jambo muhimu katika sera ya China kuhusu ufunguaji mlango, na mwaka huu China itaongeza nguvu ya kuvutia uwekezaji.

    Mwezi Januari mwaka huu thamani ya matumizi ya fedha za kigeni ya China ilipungua kwa asilimia 9.2. Katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Baraza la serikali la China, Bw. Gao Hucheng alipozungumia kama hii ni ishara ya "kuondoka kwa uwekezaji kutoka China", anasema:

    "Mwaka jana thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja ilipungua kwa kiasi kikubwa duniani, na thamani ya matumizi ya fedha za kigeni ya China ilikuwa RMB yuan bilioni 813.2, hili ni ongezeko la asilimia 4.1 kuliko mwaka uliotangulia. Ongezeko la fedha za kigeni katika sekta ya utengenezaji wa dawa lilifikia asilimia 55.8, katika sekta ya vifaa vya matibabu lilifikia asilimia 95, na katika sekta ya utoaji wa huduma za teknolojia za hali ya juu lilifikia asilimia 86.1. Tukiangalia kupungua kwa fedha za kigeni katika mwezi Januari mwaka huu, naona tunapaswa kupima mwelekeo wa hali ya uvutiaji wa fedha za kigeni katika muda wa miezi mitatu ama muda mrefu zaidi, na si mwezi mmoja tu. Hususan mwezi Januari kulikuwa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, takwimu za mwezi huu hazifai kuchukuliwa kama kipimo cha mwelekeo wa uwepo wa fedha za kigeni wa China."

    Bw. Gao Hucheng ameongeza kuwa mwaka 2017 China itaongeza nguvu katika kuvutia fedha za kigeni, na kuendelea kupunguza vikwazo kwa uwekezaji wa nchi za nje, kuzidi kurahisisha hatua za kufanya uwekezaji, na kuweka mazingira ya biashara yenye usawa, yaliyo wazi na yanayoweza kukadiriwa.

    Mwaka 2016, uwekezaji wa China katika nchi za nje ulipata ongezeko la kasi, na uwekezaji wa moja kwa moja kwenye sekta isiyo ya fedha katika nchi za nje ulizidi dola za kimarekani bilioni 170, hili ni ongezeko la asilimia 40. Bw. Gao Hucheng anasema:

    "Mwaka 2017 tutazidi kurahisisha hatua za kuidhinisha uwekezaji katika nchi za nje, kuboresha huduma za umma, na kuimarisha usimamizi katika sekta hiyo. Pia China itaimarisha majadiliano na ushirikiano na nchi za nje, ili kuweka mazingira mazuri kwa mfumo wa sheria za kimataifa kwa ajili ya kampuni zinazowekeza katika nchi za nje, ili kulinda haki za kampuni hizo kwa kufuata kanuni na sheria."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako