• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watafiti wasema New Zealand iko kwenye bara jipya lisilojulikana na watu

  (GMT+08:00) 2017-02-22 16:34:35

  Tovuti ya gazeti la GSA Today imetoa ripoti ikisema New Zealand iko kwenye bara jipya lisilojulikana na watu ambalo linatakiwa kupewa jina la bara la Zealandia.

  Watafiti wa idara ya jiografia na sayansi ya nyuklia ya New Zealand wamesema bara la Zealandia lina ukubwa wa kilomita milioni 4.9 za mraba, ambao ni theluthi mbili ya ukubwa wa Australia. Asilimia 94 ya bara hili liko chini ya bahari ya Pasifiki. Bara hili liliwahi kuwa sehemu moja ya bara la kale la Gondwana, na kuchukua asilimia 5 ya bara la Gondwana. Katika miaka milioni 100 iliyopita, bara la Zealandia lilitengana na bara la kale la Gondwana, na katika miaka milioni 80 iliyopita lilitengana na bara la Australia.

  Bara la Zealandia linaendana na vigezo vyote vya bara, vikiwemo urefu mkubwa zaidi kuliko maeneo yaliyoko kando yake, hali ya kipekee ya kijiografia, mpaka dhahiri, na tabaka nene la juu. Bara hili lina sehemu tatu za nchi kavu, zikiwemo visiwa vya kusini na kaskazini vya New Zealand na New Caledonia.

  Katika miaka mingi iliyopita, wanasayansi wamekuwa wakikusanya ushahidi unaoweza kuthibitisha kuwepo kwa bara la Zealandia. Hivi sasa hakuna idara yoyote ya sayansi iliyothibitisha rasmi utafiti huo, lakini mwandishi mkuu wa ripoti hiyo Bw. Nick Mortimer amesema anatarajia bara hili jipya litathibitishwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako