• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Budapest kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuandaa michezo ya Olympiki mwaka 2024

    (GMT+08:00) 2017-02-23 09:10:25

    Msemaji wa serikali ya Hungary amethibitisha kuwa Budapest imeamua kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuandaa michezo ya Olympiki mwaka 2024. Zaidi ya watu 260,000 wanalalamika dhidi ya hatua ya kuwa mwenyeji, wakisema pesa zinafaa kutumiwa katika mahospitali na mashule.

    Los Angeles na Paris pia ni miji inayowania kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya Hamburg kujitoa mwaka 2015 ikifuatiwa na Rome mwaka mmoja baadaye. Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC itachagua mshindi kwenye kura zitakazopigwa Lima, Peru, September 2017.

    Msemaji wa serikali ya Hungary Zoltan Kovacs amesema uamuzi wa kujiondoa ulifikiwa baada ya mkutano kati ya waziri mkuu Viktor Orban, Meya wa Budapest Istvan Tarlos na kamati ya Olimpiki ya Hungary. Hata hivyo chama tawala Fidesz, kimesema uamuzi huo umekuja ili kuepusha nchi hiyo kushuka hadhi yake kimataifa kwa vile ilikuwa na nafasi ndogo ya kushinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako