• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya nyumba katika robo ya kwanza ya mwaka huu yakadiriwa kupata utulivu

    (GMT+08:00) 2017-02-23 17:02:37

    Ofisa wa Wizara ya nyumba na ujenzi wa miji na vijiji ya China, amesema inakadiriwa kuwa mwaka huu bei ya nyumba katika robo ya kwanza itapata utulivu, na serikali ina uwezo na mbinu za kuhakikisha soko la nyumba linapata maendeleo kwa utulivu.

    Katika mkutano na waandishi wa habari wa Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China, bei ya nyumba ni moja ya masuala yanayofuatiliwa zaidi. Waziri wa nyumba na ujenzi wa miji na vijiji ya China Bw. Chen Zhenggao anakadiria kuwa bei ta nyumba katika robo ya kwanza ya mwaka huu itakuwa tulivu. Akizungumzia mwelekeo wa bei ya nyumba kote nchini kwa mwaka 2017 anasema:

    "Ingawa mwaka huu soko la nyumba bado litakabiliwa na changamoto nyingi, lakini naona pia litapata fursa zaidi, na tuna uwezo na mbinu za kuhakikisha soko la nyumba linapata maendeleo kwa utulivu."

    Kabla ya hapo, takwimu kutoka Idara ya takwimu ya China zimeonesha kuwa, katika mwezi Januari, bei ya nyumba katika miji mikubwa inalingana na ya mwezi uliopita. Bei ya nyumba katika miji ya ngazi ya pili iliongezeka kwa asilimia 0.1, kiasi hicho kimepungua kwa asilimia 0.1 kuliko mwaka jana. Bei ya nyumba katika miji mikubwa imepungua kwa miezi minne mfululizo ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, na bei ya nyumba katika miji ya ngazi ya pili imepungua kwa miezi miwili mfululizo ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

    Bw. Chen Zhenggao amesema, mwaka huu kazi kuu ni kuzuia ongezeko la kupita kiasi kwa bei ya nyumba katika miji muhimu, na mwelekeo wa kuongezeka na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa bei ya nyumba, kutatua ziada kubwa kupita kiasi kwa nyumba katika miji ya ngazi ya tatu na nne, na kuendelea kuwahimiza wakulima wanaofanya vibarua katika miji kununua nyumba mijini. Bw. Chen anasema:

    "Inapaswa kuinua kiwango cha utoaji wa huduma za matibabu na elimu, pamoja na mawasiliano ya miundo mbinu kati ya miji ya ngazi ya tatu na nne na kati ya miji mikubwa, na kuhimiza usawa wa utoaji wa huduma za umma. Wakulima wanaofanya vibarua mijini wanatakiwa kupewa huduma za umma zinazolingana na wakazi wa miji mikubwa, huu ni mvuto muhimu kwa wakulima wanaofanya kazi mijini, pia ni masharti ya lazima yanayohitaji kutolewa na serikali."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako