• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mageuzi ya kampuni za serikali yatekelezwa kwa hatua madhubuti nchini China

    (GMT+08:00) 2017-02-24 18:00:29

    Katika Mkutano wa kwanza wa baraza la maendeleo kuhusu mageuzi ya kampuni ya China lililofanyika tarehe 23, mkurugenzi wa Kamati ya rasilimali za taifa katika baraza la serikali la China Bw. Xiao Yaqing amesema, baada ya kufanyika kwa mageuzi ya kina, ufanisi wa uendeshaji wa kampuni za serikali umeongezeka dhahiri, hatua za uvumbuzi pia zimezidi kuimarishwa, hali ambayo imehimiza mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa. Pili Mwinyi ana maelezo zaidiā€¦

    Kampuni za serikali zikiwa sehemu muhimu katika uchumi wa soko wa China, mageuzi yake siku zote ni kiini cha mageuzi ya mfumo wa uchumi nchini China. Katika muda mrefu uliopita, bado kuna kasoro katika usimamizi, uchaguaji wa wataalamu na utoaji wa mishahara ndani ya kampuni za serikali. Akizungumzia hali hiyo naibu katibu mkuu wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Fan Hengshan anasema:

    "Hivi sasa mfumo wa kampuni za kisasa bado haujakamilika, majukumu ya uendeshaji na uwekezaji bado hayajakamilika, na ufanisi wa uendeshaji wa mitaji ya serikali ni mdogo. Kazi muhimu ya kutatua masuala hayo ni kuhimiza mageuzi ya kampuni hizo."

    Katika miaka kadhaa iliyopita, serikali ya China imetekeleza mageuzi ya kina na kuanzisha utaratibu wa uendeshaji unaolingana na sheria ya uchumi wa soko na maendeleo ya kanuni, hatua hii imehimiza kampuni za serikali kupata uwezo mkubwa zaidi wa ushindani. Kampuni nyingi za serikali kuu pia zimeanzisha bodi ya wakurugenzi inayoundwa na wakurugenzi kutoka nje ya kampuni hizo, na mamlaka ya bodi hiyo ya kuwajiri wafanyakazi, kutoa uamuzi muhimu na kugawanya mishahara zimeanza kutekelezwa hatua kwa hatua. Mkurugenzi wa Kamati ya rasilimali ya taifa katika Baraza la serikali la China Bw. Xiao Yaqing anasema:

    "Hadi sasa Mageuzi ya kampuni na wenyehisa yamepata maendeleo kwa pande zote, mageuzi ya umilikaji mseto yanatekelezwa kwa hatua madhubuti. Mabadiliko ya mfumo wa kampuni yanahimiza ukamilifu wa muundo wa usimamizi wa kampuni na kuongezeka kwa ufanisi uendeshaji wa fedha."

    Katika kipindi kijacho, kampuni za serikali zitafuata kanuni za kukamilisha usimamizi, kuboresha utaratibu wa kutia moyo, na kuongeza ufanisi, na kupiga hatua halisi katika sekta za nishati ya umeme, mafuta ya petroli, gesi, reli, ndege za abiria, na viwanda vya kijeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako