• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusaidia asilimia 25 ya watu maskini kuondokana na umaskini mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-02-24 19:23:50

    Naibu mkurugenzi wa ofisi ya kuwasaidia watu kuondokana na umaskini ya Baraza la serikali la China Bw. Ou Qingping, leo hapa Beijing amesema hivi sasa nchini China bado kuna watu maskini milioni 40. Na mwaka huu China lazima itawasaidia watu milioni 10 kuondokana na umaskini, hivyo inaweza kuhakikisha utimizaji wa lengo la kuwasaidia watu wote kuondokana na umaskini kabla ya mwaka 2020. Hii inamaanisha kuwa mwaka huu asilimia 25 kati ya watu hao wataondokana na umaskini.

    Bw. Ou Qingping amesema, mwaka huu China itachukua hatua tatu ili kuongeza nguvu ya kupunguza umaskini. Kwanza, China itaunganisha raslimali na kuongeza kazi ya kupunguza umaskini. Pili, China itakamilisha utaratibu wa wajibu, na kuinua kiwango cha ufanisi cha matumizi ya fedha. Tatu, China itaimarisha ukaguzi na usimamizi kwa kazi ya kupunguza umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako