• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kutafuta chakula kumewafanya binadamu na nyani wawe na uwezo mkubwa zaidi wa kuona rangi mbalimbali

  (GMT+08:00) 2017-02-27 19:22:34

  Kwenye macho ya binadamu na baadhi ya nyani kuna aina tatu za seli za kuhisi mwanga zenye umbo la koni, ambazo zinawawezesha kuona rangi mbalimbali. Baadhi ya vipofu wa rangi hawawezi kutofautisha rangi nyekundu na kijani, kwani macho yao yanakosa seli zinazohisi mwanga mwekundu au mwanga wa kijani.

  Watafiti wanaona uwezo mkubwa zaidi wa kutofautisha rangi mbalimbali umewasaidia binadamu wa kale na nyani kugundua matunda kwa urahisi zaidi misituni. Ili kuthibitisha maoni hayo, wakafanya majaribio kwa kima aina ya rhesus, ambao baadhi yao wana aina tatu za seli za kuhisi mwanga kwenye macho yao, na wengine wana aina mbili tu.

  Watafiti wamechunguza vitendo zaidi ya elfu 20 vya kima zaidi ya 80 vya kutafuta matunda kutoka kwenye aina 30 za miti katika kisiwa cha San Diego, Pueto Rico, na wakagundua kuwa kima wenye aina tatu za seli za kuhisi mwanga wanaweza kutafuta matunda kwa muda mfupi zaidi kuliko wale wenye aina mbili za seli. Matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa mahitaji ya kutafuta chakula yamewafanya binadamu wa kale na baadhi ya nyani wawe na uwezo mkubwa zaidi wa kuona rangi mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako