• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Leicester City yaibamiza Leverpool 3-1

    (GMT+08:00) 2017-02-28 08:45:30

    Timu ya Leicester City imejikokota na kupanda hadi nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuibamiza Liverpool kwa mabao 3-1.

    Leicester city walionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo na mabao mawili kutoka kwa Jamie Vardy na moja lilifungwa na Danny Drinkwater yalitosha kabisa kuididimiza Liverpool.

    Katika mchezo huo, Leicester walicheza chini ya kocha msaidizi Craig Shakespeare, aliyechukua mikoba ya Ranieri.

    Liverpool ambao wangeweza kupanda hadi nafasi ya tatu iwapo wangepata ushindi, sasa wamepoteza mechi tano kati ya saba walizocheza katika michuano yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako