• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanajimu wagundua mfumo wa nyota unaofanana sana na mfumo wa jua

  (GMT+08:00) 2017-02-28 15:24:10

   

  Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA hivi karibuni ilitangaza kuwa kikundi cha wanajimu cha kimataifa kimegundua mfumo wa nyota wenye sayari 7 ambao uko katika umbali wa miaka 40 ya kusafiri mwanga kutoka duniani. Wanajimu wamesema mfumo huo unaofanana sana na mfumo wa jua ni mahali pazuri pa kutafuta viumbe nje ya dunia.

  Naibu mkurugenzi wa NASA Bw Thomas Zurbuchen amesema ugunduzi huo unathibitisha lile swala la si kama kuna uwezekano wa kutafuta sayari inayofanana na dunia au la, bali ni lini itagunduliwa sayari hiyo.

  Kikundi cha wanajimu kikitumia darubini ya Spitzer ya NASA na njia nyingine mbalimbali, kiligundua kuwa kuna sayari 7 zinazoundwa na miamba yenye ukubwa unaofanana na dunia katika mfumo wa nyota kibete iitwayo TRAPPIST-1. Miongoni mwa sayari hizi, tatu ziko katika ukanda wenye mazingira yanayofaa kuwepo kwa viumbe, na huenda zote zina maji.

  NASA imesema huu ni mfumo wa nyota uliogunduliwa na binadamu mpaka sasa ambao una sayari nyingi zaidi katika ukanda wenye mazingira yanayofaa kuwepo kwa viumbe.

  Utafiti huo uliofanywa na wanasayansi wa Marekani, Ubelgiji na Uingereza umetolewa kwenye gazeti la Nature.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako