• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka kampuni ya Lotte ifuate sheria na kanuni nchini China

    (GMT+08:00) 2017-02-28 18:37:59

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inayakaribisha makampuni ya nchi mbalimbali kufanya uwekezaji na kuanzisha shughuli zao nchini China, na siku zote inaheshimu na kulinda maslahi halali ya makampuni hayo.

    Geng amesema hayo alipokuwa akijibu swali kama China itaiadhibu kampuni ya Lotte ya Korea Kusini kufuatia kampuni hiyo na wizara ya ulinzi ya Korea Kusini kusaini makubaliano ya kubadilishana ardhi kwa ajili ya ujenzi wa mfumo wa THAAD wa Marekani.

    Akizungumia makubaliano hayo, Geng amesema China inapinga kithabiti uwekaji wa mfumo huo nchini Korea Kusini, na itachukua hatua zinazohitajika kulinda maslahi ya kiusalama wa China. Ameongeza kuwa, China inazihimiza pande husika kujali maslahi na mambo yanayofuatiliwa na China, kusimamisha kuweka mfumo huo, ili zisifanye makosa makubwa zaidi.

    Mapema leo, Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini ilisaini makubaliano ya kubadilishana ardhi na kampuni ya Lotte ili kuweka mfumo wa THAAD. Mwezi Julai mwaka jana, Korea Kusini na Marekani zilitangaza uamuzi wa kupeleka betri moja ya THAAD nchini Korea Kusini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako