Mshambuliaji huyo wa DR Congo mwenye umri wa miaka 31 ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Dynamo Kiev alibadilishwa wakati wa sare ya 1-1 dhidi ya Burnley. Hull pia imethibitisha kuwa jeraha la goti alilopata beki Harry Maguire wakati wa mechi dhidi ya Burnley sio baya sana zaidi ya ilivyodhaniwa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda akawa tayari ameshapona kwa safari ya kueleka Leicester City siku ya Jumamosi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |