Bunge la 12 la Umma la China leo hapa Beijing limeitisha mkutano wake wa tano, ambao umehudhuriwa na rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine wa Chama na serikali.
Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, Waziri mkuu wa China Li Keqiang ametoa ripoti ya kazi zilizofanywa na serikali mwaka uliopita, na mipango ya kazi za kiutawala kwa mwaka huu. Bw. Li ameeleza jinsi China,ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, inavyoendelea kuwa injini ya ukuaji wa uchumi wa dunia, jinsi ya kupata maendeleo mapya katika kuimarisha kwa kina mageuzi, na jinsi viongozi wa serikali watakavyowahudumia wananchi vizuri zaidi kwenye sekta za afya, nyumba na ulinzi wa mazingira.
Siku chache zijazo, wabunge wapatao elfu 3 watajadili ripoti ya kazi za serikali na kuipigia kura wakati wa ufungaji wa mkutano huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |