• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya kazi nzuri za kidiplomasia mwaka jana

    (GMT+08:00) 2017-03-05 10:17:39

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amesema mwaka jana, China ilifanya kazi nzuri za kidiplomasia kwa umaalum wa kichina.

    Bw. Li ameyasema hayo kwenye hotuba yake ya ripoti ya kazi za serikali aliyotoa kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China ulioanza leo hapa Beijing. Amesema rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine wa serikali walifanya ziara katika nchi nyingi na kuhudhuria mikutano mbalimbali ukiwemo mkutano usio rasmi wa viongozi wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi la Asia na Pasifiki APEC, mkutano wa kilele wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai SCO, mkutano wa wakuu wa nchi za BRICS, mkutano wa kilele kuhusu usalama wa nyuklia, na mikutano ya ngazi ya juu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

    Wakati huohuo, China pia imeimarisha uratibu na ushirikiano na nchi kubwa duniani, kusukuma mbele ushirikiano wa kina na nchi jirani, kuongeza urafiki na nchi zinazoendelea, na kufanya mawasiliano kwa karibu na mashirika mbalimbali ya kimataifa, ukiwemo Umoja wa Mataifa.

    Bw. Li ameongeza kuwa, China, imefanya kazi za kiujenzi kwenye masuala ya kimataifa na kikanda na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako