• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inapenda kujenga amani, kuchangia maendeleo na kulinda utaratibu wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-03-05 11:07:13

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema China inapenda kujenga amani, kuchangia maendeleo na kulinda utaratibu wa kimataifa

    Bw. Li amesema China itafuata kithabiti njia ya kujiendeleza kwa amani, kulinda hadhi na ufanisi wa mfumo wa pande nyingi, kupinga aina zote za sera za kujilinda, kushiriki kwa kina kwenye mchakato wa usimamizi wa dunia, na kufanya uchumi wa dunia uendelee kwa masikilizano, manufaa ya pamoja, haki na uhahihi.

    Pia amesema China inahimiza na kujenga utaratibu wa uhusiano kati ya nchi kubwa ulio na utulivu na maendeleo yenye uwiano, kujenga mazingira ya kirafiki na maendeleo ya pamoja na nchi jirani, kuinua kiwango cha ushirikiano na nchi nyingine zinazoendelea, na kutoa ufumbuzi wa kiujenzi kwa masuala ya kimataifa na kikanda.

    Ameongeza kuwa, China inapenda kushirikiana na jamii ya kimataifa kujenga uhusiano wa kimataifa unaotoa kipaumbele kwa ushirikiano na kutoa mchango mpya kwa ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako