• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanahabari wa Shirika la utangazaji la Kenya KBC Bw Eric Biegon afuatilia maendeleo ya mkutano wa bunge

    (GMT+08:00) 2017-03-05 15:54:32

    Kikao cha tano cha bunge la 12 la umma la China kimefunguliwa leo asubuhi hapa Beijing. Waziri Mkuu wa China Bw Li Keqiang amewasilisha ripoti ya kazi za serikali kwa mwaka huu, ikitaja mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na makadirio ya ongezeko la uchumi kupungua kutoka asilimia 6.7 ya mwaka jana hadi asilimia 6.5.

    Mwanahabari wa Shirika la utangazaji la Kenya KBC Bw Eric Biegon anayefuatilia maendeleo ya mkutano wa bunge, jana alianza kuhudhuria vikao vya utangulizi akifuatilia kama kupungua kwa ongezeko la uchumi kwa China kunaweza kumaanisha kupungua kwa misaada na uwekezaji kwa bara la Afrika. Leo amehudhuria ufunguzi wa mkutano wa bunge na ameongea na mwenzetu Fadhili Mpunji muda mfupi baada ya hotuba ya ripoti ya kazi iliyosomwa na waziri mkuu.

     

     


    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako