Rais Xi Jinping wa China amesema China itaendelea na sera ya kufungua mlango, na kufanya biashara na uwekezaji viendelee kuwa huria.
Rais Xi Jinping ametoa kauli hiyo kwenye mjadala na wajumbe kutoka mji wa Shanghai wanaohudhuria mkutano wa bunge unaoendelea kufanyika hapa Beijing.
Amesema mji wa Shanghai unatakiwa kuwa mfano wa mageuzi na ufunguaji mlango, kufanya mageuzi zaidi kwenye maeneo yake maalum ya biashara huria, kuhimiza uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, kuboresha usimamizi wa kijamii, na kusimamia chama kwa hatua kali.
Mji wa Shanghai ni mwenyeji wa eneo la kuwanza la biashara huria nchini China lililoanzishwa mwaka 2013, ambalo ni kituo cha kufanya majaribio ya sera mpya, ikiwemo utaratibu wa usimamizi wa uwekezaji kutoka nje, unaoamua ni sekta gani wawekezaji kutoka nje wanaweza kuwekeza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |