Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha Kikomunisti cha China na katibu wa kamati ya ukaguzi wa nidhamu ya chama Bw. Wang Qishan, jana aliposhiriki kwenye mjadala na wajumbe wa Beijing wanaohudhuria mkutano wa bunge la umma la China, alisisitiza umuhimu wa kutafuta njia yenye ufanisi ya usimamizi wa chama.
Amesema usimamizi wa chama unahusiana na kushikilia na kuimarisha uongozi wa chama, kuinua uwezo wake wa utawala na kiwango cha usimamizi, kwa hivyo kuna haja ya kuzidisha mageuzi ya mfumo wa ukaguzi na usimamizi wa taifa, na kujenga utaratibu wa kupambana na ufisadi unaoongozwa na chama.
Ameongeza kuwa, mageuzi ya mfumo wa usimamizi na ukaguzi yana umuhimu wa kisiasa, lengo lake ni kuimarisha uongozi wa chama katika mapambano dhidi ya ufisadi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |