Mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa la China Bw. He Lifeng leo hapa Beijing amesema, katika miaka mitatu iliyopita, uwekezaji uliofanywa na China katika nchi za Ukanda wa kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri Baharini umezidi dola za kimarekani bilioni 50.
Bw. He amesema ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unaendelea kwa kasi, pia umepata mafanikio makubwa kuliko ilivyotarajiwa. Amesema pendekezo la China kuhusu "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limeungwa mkono na zaidi ya nchi na mashirika ya kimataifa 100, na China imesaini makubaliano mbalimbali ya ushirikiano na serikali za nchi nyingine, na makubaliano kadhaa ya ushirikiano na mashirika ya kimataifa.
Bw. He pia amejulisha kuwa mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu "Ukanda mmoja na Njia moja" utafanyika hapa Beijing mwezi Mei mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |