• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UEFA Champions Ligi: Leo Arsenal itaweza kusonga mbele?

    (GMT+08:00) 2017-03-07 08:13:19

    Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA Champions Ligi zinaanza kuchezwa Leo Jumanne Machi 7 kwa Mechi 2.

    Huko Emirates Jijini London, Wenyeji Arsenal wanakutana na Bayern Munich. Mechi ya kwanza ilichezwa huko Germany.

    Ili kufuzu kuingia Robo Fainali, Arsenal wanapaswa kushinda 4-0 ama kwa idadi nyingine ya mabao ili mradi tofauti ya Magoli iwe 4-0.

    Mechi ya Pili leo ni huko Naples Italy, wakati Napoli itarudiana na Mabingwa Watetezi Real Madrid huku wakihitaji ushindi wa Bao 2-0 kwa vile walichapwa 3-1 huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Spain kwenye Mechi ya Kwanza.

    Jumatano Machi 8 zipo Mechi nyingine 2 za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kati ya Barcelona na Paris Saint Germaine.

    Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitakamilika Wiki ijayo, Machi 14 na 15, kwa Mechi nyingine 4 ili kutoa Washindi watakaocheza Robo Fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako