Mchumi Bw. Li Yining, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, amesema ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu huenda litazidi asilimia 6.5.
Bw. Li Yining amesema,
"Kama tunavyojua, China iko katika kipindi cha mageuzi, inatakiwa kuhamisha vipaumbele vyake kutoka kuzingatia kasi ya ongezeko na ukubwa wa uchumi, hadi kwenye ufanisi na ubora. Ndiyo maana mageuzi ya muundo wa uchumi bado yanaendelea. Ukiona uchumi wa China umefikia kwenye kipindi cha mageuzi, swali la kwanza kujiuliza ni kwamba, je mageuzi ya kimuundo yamekamilika? Jibu ni Bado hayajakamilika. Hali ya sasa nchini China inaonyesha kuwa, tunaendelea kufanya marekebisho na mageuzi ili kufika kwenye nafasi mpya."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |