Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amefanya mzungumzo na ujumbe wa mkoa wa Shangdong kuhusu ripoti ya mipango ya kazi za serikali katika Mkutano wa tano wa bunge la awamu ya 12 la umma la China.
Katika mazungumzo hayo, Li amesema, mafanikio yaliyopatikana mwaka jana nchini China yameweka msingi mzuri kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii kwa mwaka huu. Amesema lengo la ongezeko la uchumi kwa mwaka huu lililowekwa kwenye ripoti ya mpango wa kazi za serikali ni asilimia 6.5, kiasi hicho kinalingana na kanuni ya uchumi, na ongezeko la uchumi litazidi kiwango cha mwaka jana na pia kinaweza kuhakikisha utoaji wa nafasi za kutosha za ajira.
Bw. Li Keqiang pia amesema njia muhimu ya kuhakikisha ongezeko la mwendo wa kati na wa kasi wa uchumi ni kuhimiza mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa, kuimarisha uvumbuzi, kuhimiza uundwaji upya wa viwanda na upandaji wa madaraja ya uchumi. Pia amesisitiza kuwa kuboreshwa kwa maisha ya wananchi ni kipimo muhimu cha matokeo ya utekelezaji wa mipango hiyo
.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |