• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kuchangia utulivu, ukuaji, amani, utawala wa dunia

    (GMT+08:00) 2017-03-08 11:18:10

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema China itaendelea kuwa nanga ya utulivu wa kimataifa, na injini ya ukuaji wa kimataifa, mtetezi wa amani na maendeleo na kuchangia utawala bora kimataifa.

    Wang ameleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano unaoendelea wa mwaka wa Bunge la Umma la China hapa Beijing.

    Wakati huo huo Bwana Wang ameeleza kuwa mpango wa Ukanda Mmoja na Njia Moja umekuwa jukwaa bora kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa wenye matarajio makubwa duniani.

    Wakuu zaidi ya 20 wa nchi na serikali, zaidi ya viongozi 50 wa mashirika ya kimataifa, zaidi ya maafisa 100 wa wizara mbalimbali pamoja na wajumbe kutoka nchi mbalimbali watahudhuria kongamano kubwa la Ukanda Mmoja na Njia Moja kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa litakalofanyika mwezi Mei mwaka huu mjini Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako