• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China asema sifa tatu mpya zinajitokeza katika ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-08 11:27:41

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema sifa tatu mpya zinajitokeza katika ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika.

    Bw. Wang ameyasema hayo akijibu swali la mwandishi wa habari Theopista Nsanzugwanko kutoka Gazeti la Habarileo la Tanzania kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika. Amesema hivi sasa ushirikiano kati ya pande hizo mbili umebadilika kutoka kuongozwa na serikali hadi kuamuliwa na soko, kutoka biashara ya bidhaa hadi ushirikiano wa kiviwanda na kutoka ukandarasi hadi uwekezaji.

    Pia amesema China iliwahi kuwa rafiki wa dhati wa nchi za Afrika katika juhudi zao za kujipatia uhuru, na leo China hakika itakuwa mwenzi wa kutegemeka wa kusaidia Afrika kuendeleza sekta ya viwanda, kilimo cha kisasa na kuinua uwezo wa kujiendeleza.

    Ameongeza kuwa China itatekeleza kithabiti ahadi zake kwa Afrika bila kujali jinsi hali ya kimataifa inavyobadilika. Ameongeza kuwa tayari nusu ya dola za kimarekani bilioni 60 zilizoahidiwa na China kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC zimetolewa. Wakati huohuo, miradi mbalimbali kati ya China na nchi za Afrika inatekelezwa hatua kwa hatua, ikiwemo mradi wa bandari nchini Tanzania na reli ya Mombasa na Nairobi nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako