• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kubeba wajibu zaidi badala kutafuta uongozi duniani

    (GMT+08:00) 2017-03-08 12:29:00

    China itabeba wajibu zaidi na kuchangia zaidi amani na ukuaji wa dunia badala kutarajia kuwa kiongozi wa dunia.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi leo amewaambia waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi wanaoripoti mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China hapa Beijing kuwa nchi zote kubwa kwa ndogo ziko katika hali ya usawa, na China haioni kuwa nchi kadhaa zinaweza kuziongoza nyingine. Pia amesema Umoja wa Mataifa ambao ni shirika lenye mamlaka na la kuaminika kati ya serikali unapaswa kutumia nafasi yake kwa ufanisi katika kuratibu masuala ya kimataifa kwa mujibu wa malengo na kanuni za mkataba wake.

    Ameongeza kuwa China ikiwa mjumbe wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, itatimiza kikamilifu wajibu wake kwa ajili ya amani na usalama wa kimataifa na kuchangia ukuaji wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako