• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuondoa umaskini ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2017-03-08 17:16:19

    Mkurugenzi wa ofisi ya kusaidia watu kuondokana na umaskini ya baraza la serikali la China Bw. Liu Yongfu amesema, watu wote maskini vijijini nchini China wataondokana na umasikini ifikapo mwaka 2020, kwa mujibu wa vigezo vya umaskini vya sasa.

    Amesema China itatekeleza utaratibu mkali zaidi wa ukaguzi, na kuhakikisha mafanikio halisi ya kuondoa umaskini, pia itachukua hatua ili kuhakikisha mafanikio hayo yanaweza kuthibitishwa na historia. Bw. Liu amesema vigezo vya kuondokana na umaskini kwa watu ni kuwaondolea wasiwasi kuhusu chakula, kuwapatia huduma za elimu ya lazima, matitabu ya kimsingi na usalama wa nyumba.

    Vilevile amesema utalii wa vijiji umekuwa nguvu kuu ya kuhimiza kipato cha wakulima na maendeleo ya uchumi, na katika miaka mitano iliyopita, China imewasaidia watu maskini milioni 10 kuondokana na umaskini kwa njia ya kukuza utalii wa vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako