Katika ripoti hiyo, spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang amesema, mwaka jana Kamati ya kudumu ya bunge la umma la China ilitilia mkazo katika miradi muhimu inayohusu mageuzi, maendeleo na utulivu, kuboresha ubora wa utungaji wa sheria, na kutekeleza hatua kwa hatua sheria kadhaa muhimu. Amesema mwaka huu, kamati hiyo itarekebisha sheria ya usimamizi wa kiutawala kuwa kuwa sheria ya usimamizi ya taifa, na pia sheria mbalimbali zinazohusu jamii, utamaduni na ikolojia zitatungwa au kukamilishwa. Bw. Zhang Dejiang pia amesisitiza kuwa kazi kuu ya kamati hiyo mwaka huu itakuwa ni kukamilisha mfumo wa sheria kwa kufuatia mfumo mpya wa maendeleo wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |