• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magufuli azindua uwanja wa ndegevita Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-03-08 19:42:52

    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, amezindua uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere uliofanyiwa ukarabati baada ya miundombinu ya uwanja huo kuharibika.

    Katika hotuba yake Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Tanzania (JWTZ) kwa kazi kubwa linayofanya na pia akamshukuru Rais wa China Xi Jinping na Serikali yake kwa msaada mkubwa iliyoutoa kujenga uwanja huo.

    Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing amesema kujengwa kwa uwanja huo kumeimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na China na amempongeza Magufuli kwa kuendeleza uhusiano huo.

    Mbali na kuzindua uwanja huo Magufuli alishuhudia maonesho ya ndege za kivita zilizorushwa kwa mbinu mbalimbali za kivita, ili kutoa heshima

    Jenerali Mabeyo amesema kuwa uwanja huo ni miongoni mwa viwanja bora zaidi duniani kwa sasa na una uwezo wa kutumiwa na ndege za aina zote zilizo huku akibainisha kuwa pamoja na ndege za kivita pia unaweza kutumiwa na ndege za kawaida za abiria kwa dharula.

    Aidha, Magufuli ameahidi kujenga barabara ya lami ya kuunganisha kamandi ya Jeshi la anga ya Ngerengere na barabara kuu ya Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako