• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 2 wa wajumbe wote katika Mkutano wa tano wa bunge la umma la China la awamu ya 12 wafanyika

    (GMT+08:00) 2017-03-08 21:18:39

     

    Mkutano wa 2 wa wajumbe wote wa mkutano wa tano wa bunge la umma la China la awamu ya 12 umefanyika leo, ambapo spika wa bunge hilo Bw. Zhang Dejiang alitoa ripoti ya kazi za Kamati ya Kudumu ya bunge la umma la China.

    Katika ripoti hiyo, Zhang Dejiang amesema, mwaka jana Kamati ya kudumu ya bunge la umma la China ilitilia mkazo katika miradi muhimu inayohusu mageuzi, maendeleo na utulivu, kuboresha ubora wa utungaji wa sheria, na kutekeleza hatua kwa hatua sheria kadhaa muhimu. Amesema mwaka huu, kamati hiyo itarekebisha sheria ya usimamizi wa kiutawala kuwa kuwa sheria ya usimamizi ya taifa, na pia sheria mbalimbali zinazohusu jamii, utamaduni na ikolojia zitatungwa au kukamilishwa. Bw. Zhang pia amesisitiza kuwa kazi kuu ya kamati hiyo mwaka huu itakuwa ni kukamilisha mfumo wa sheria kwa kufuatia mfumo mpya wa maendeleo wa China.

    Mbali na hayo, mkutano huo umesikiliza ufafanuzi kuhusu mswada wa sheria ya umma, orodha ya majina ya wajumbe wa bunge la umma la China la awamu ya 13, na uamuzi kuhusu uchaguzi, pamoja na njia za kufanya uchaguzi wa wajumbe wa bunge la umma la China la awamu ya 13 wa mikoa ya utawala maalumu ya Hong Kong na Macao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako