Viongozi wa ngazi ya juu wa China akiwemo rais Xi Jinping, waziri mkuu Bw. Li Keqiang, spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang, na mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng, kwa nyakati tofauti wameshiriki katika mazungumzo ya ujumbe wa mikoa mbalimbali kuhusu ripoti ya mipango ya kazi za serikali katika Mkutano wa tano wa bunge la umma la China wa awamu ya 12.
Rais Xi alipozungumza na ujumbe wa mkoa wa Sichuan amepongeza juhudi zilizofanywa na mkoa huo katika mwaka mmoja uliopita, pia amesisitiza kuwa inapaswa kutilia mkazo mkubwa katika sekta ya kilimo, kusukuma mbele mageuzi ya kimuundo ya mambo ya kilimo kwenye utoaji wa bidhaa, kuondoa umasikini vijijini ifikapo mwaka 2020. Pia amezungumzia kuimarisha uvumbuzi, kuweka mazingira mazuri ya kisiasa, kufanya mipango mizuri ya kuhakikisha ongezeko kwa hatua madhubuti, kuhimiza mgeuzi, kurekebisha muundo ili kuwanufaisha wananchi na kuepukana na matishio mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |