• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barcelona wafanya maajabu dhidi ya Paris Saint Germain Klabu Bingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-03-09 08:57:40

    Barcelona wamebirua matokeo ya kutinga nusu fainali kwa kuichakaza Paris Saint Germain mabao 6-1 katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya. Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliocharazwa kwenye dimba la Nou Camp.

    Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1. Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris. Hatua ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya UEFA, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.

    Katika mchezo mwingine, Pierre Emerick Aubameyang alipachika 'hat trick' na kuipeleka Borussia Dortmund katika robo fainali dhidi ya Benfica. Borussia Dortmund wameshinda kwa jumla ya magoli 4-1 katika mechi mbili walizocheza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako