Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria mjadala na wajumbe wa mkoa wa Sichuan, wanaohudhuria mkutano wa bunge la umma unaoendelea hapa Beijing, na kusisitiza kuwa China inahitaji mfumo wenye ufanisi wa kudumu wa kuondoa umaskini.
Sichuan ni moja ya mikoa inayosumbuliwa na tatizo la umaskini, kwa sasa idadi ya watu maskini mkoani humo imefikia milioni 2.72 kutoka milioni 7.5 ya mwaka 2012, ikiwa imepungua kutoka asilimia 11.5 hadi asilimia 4.3.
Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, inapaswa kutoa kipaumbele kwa kazi ya kupambana na umaskini katika maeneo ya makabila ya wayi na watibet. Amesema:
"kwa sasa jambo muhimu kwenye mapambano dhidi ya umaskini ni kuwalenga kwa usahihi watu wenye mahitaji na kufuatilia madiwani, mchakato mzima unahitaji usahihi na umakini, ili kuthibitisha bayana ni nani watakaosaidiwa, nani atatoa msaada huu, jinsi anavyosaidia na vigezo vya kuhakikisha walengwa wanaondokana na umaskini, kazi hizo zote zinahitaji umakini mkubwa. Kuzuia walengwa kurudi tena kwenye umaskini kuna umuhimu sawa na juhudi za kuwatoa kwenye umaskini, ambako kunakuhitaji kuimarisha uwezo wao wa kujiendeleza."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |