• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China wahudhuria mijadala na wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa Bunge la Umma la China

    (GMT+08:00) 2017-03-09 21:27:55

    Viongozi wa ngazi ya juu wa China akiwemo Waziri mkuu Bw. Li Keqiang, spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang, na mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng wamehudhuria mijadala ya wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa Bunge la Umma la China.

    Bw. Li Keqiang alipohudhuria mjadala wa wajumbe kutoka mkoa wa Shaanxi alisema, anatumai mkoa huo utahimiza maendeleo ya uchumi na jamii, kukuza mageuzi katika sekta mbalimbali, na kuweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha na kuboresha maisha ya wananchi. Pia alisema mkoa huo uongeze juhudi katika kutatua matatizo ya maisha ya wananchi yakiwemo miundo mbinu, elimu, matibabu na ikolojia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako