Mwanauchumi na mtaalamu wa maswala yanayohusu China Bw. Joshua Mukhenya amesema, uhusiano kati ya China na nchi za Afrika umekuwa mzuri sana kutokana na msaada unaotolewa na China kwa nchi za Afrika. Ushirikiano katika nyanja ya uchumi, fedha, miundombinu mfano barabara, hospitali za hapa Uganda unafanywa kati ya pande hizo mbili.
Bw. Joshua Mukhenya ameeleza kuwa, utekelezaji huu wa miradi ndio misingi ya uchumi uonaleta manufaa kwa nchi za Afrika, kupitia miradi hii wananchi wa hali ya chini wameweza kupata ajira. Changamoto ambayo naona China inakumbana nazo katika kutekeleza miradi hii katika nchi za Afrika kama Uganda ni lugha, watu wengi katika bara la Afrika hawajui kuzungumza kichina hivyo hutumia ishara ya mikono kuwasiliana naona kwakuwa Chuo cha Makerere kimesema kitaanzisha mafunzo ya lugha ya kichina hii itasaidia na kuleta mafanikio makubwa sana. Nchi za Afrika zitanufaika zaidi na China kutokana na China kutotoa masharti mengi sana kwa mikopo yake kulinganisha na nchi nyingine za magharibi.
Ameongeza kuwa, ushawishi wa China katika sekta ya biashara barani Afrika utasaidia fedha za nchi nyingi za Afrika kuwa imara, vilevile vijana wengi wamepata ajira kutokana na miradi ambayo China imewekeza na inaendelea kuwekeza barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |