• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutumia bilioni 1.5 kuwa upanuzi wa barabara

    (GMT+08:00) 2017-03-10 19:14:22

    Serikali ya Kenya itatumia shilingi bilioni 1.5 katika mwaka ujao wa kifedha kugharamia upanuzi wa uwanja wa ndege wa Malindi katika kaunti ya Kilifi. Katibu wa wizara ya uchukuzi Bw Irungu Nyakera amesema sehemu ya fedha hizo zitatumiwa kwa ununuzi wa ekari 200 za ardhi zitumike kwa upanuzi wa uwanja huo. Nyakera ameongeza kuwa ardhi hiyo itatumiwa kwa upanuzi wa barabara ya ndege kutua ama kupaa kutoka umbali wa kilomita 1.5 hadi 2.5. Hivi sasa uwanja huo hauwezi kupokea ndege kubwa kutokana na barabara ndogo ya kilomita 1.4 ambapo ni ndege za kubeba abiria 90 pekee ndizo zinaweza kutua. Nyakera ameongeza kuwa pindi barabara ya ndege itakapopanuliwa basi safari za ndege za moja kwa moja kutoka ulaya hadi Malindi zitaanza. Mwaka jana, serikali ya Kenya ilitoa jumla ya shilingi milioni 300 kulipa fidia kwa familia ambazo zilikuwa zikiishi katika ardhi ya hekta 25 karibu na uwanja wa ndege wa Malindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako