• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China wahudhuria mijadala na wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa Bunge la Umma la China

    (GMT+08:00) 2017-03-10 21:09:47

       

    Viongozi wa ngazi ya juu wa China akiwemo rais Xi Jinping wa China, Waziri mkuu Bw. Li Keqiang, spika wa bunge la umma la China Bw. Zhang Dejiang, na naibu waziri mkuu Bw. Zhang Gaoli wamehudhuria mijadala ya wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa tano wa Bunge la Umma la China la awamu ya 12.

    Akizungumza na wajumbe kutoka mkoa wa Xinjiang, Rais Xi Jinping amesema, inapaswa kufuata lengo kuu la kudumisha utulivu wa jamii na usalama wa kudumu, kusukuma mbele mfumo na uwezo wa utawala wa mkoa huo, na kuhimiza maendeleo ya jamii na kuboresha maisha ya watu. Pia amesema ni muhimu kulinda muungano wa taifa na kuhimiza mshikamano wa makabila, na kuimarisha masikilizano kati ya makabila mbalimbali ili kuufanya mkoa huo kupata masikilizano, maendeleo na maisha bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako