Rais Xi Jinping wa China jana alishiriki kwenye mjadala wa wajumbe kutoka mkoa wa Xinjiang wa Mkutano wa tano wa Bunge la Umma la China la awamu ya 12 ambao leo umeingia siku yake ya nane.
Katika mjadala huo, rais Xi amesisitiza kuwa mkoa wa Xinjiang unapaswa kufuata lengo kuu la kudumisha utulivu wa jamii na usalama wa kudumu, kutekeleza wazo jipya la kujiendeleza, kuhimiza maendeleo ya jamii na kuboresha maisha ya watu, kuzidi kuimarisha muungano wa taifa ili kuufanya mkoa huo kupata masikilizano, maendeleo na maisha bora.
Akizungumzia namna ya kuhimiza mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa mkoani humo, rais Xi anasema:
"Mkoa wa Xinjiang unapaswa kuimarisha viwanda vyenye sifa bora, kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu, kufanya juhudi za kulinda mazingira ya ikolojia, kuongeza nguvu katika kukinga na kupambana na uchafu wa mazingira na kuenea kwa jangwa."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |