• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa mchango mkubwa zaidi kwa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2017-03-12 11:16:44

    Balozi wa Jamhuri ya Congo nchini China Bw. Daniel Owassa amesema China itatoa mchango mkubwa zaidi kwa uchumi wa dunia.

    Balozi Owassa amesema hayo alipokuwa akizungumza kuhusu Mkutano wa Bunge la Umma la China na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China inayoendelea hapa Beijing. Amesema mwaka huu ni muhimu kwa utekelezaji wa mpango wa 13 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi na jamii wa China, pia ni muhimu wa kuimarisha mageuzi katika pande zote. Bw. Owassa amesema mwaka jana China ilichangia asilimia 30 katika ongezeko la uchumi wa dunia, na anaamini kwamba uchumi wa China utatoa mchango mkubwa zaidi katika kufufua uchumi wa dunia.

    Pia ametoa pongezi kwa uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Congo, amesema China itaunga mkono ujenzi wa eneo maalum la kiuchumi la Pointe-Noire nchini humo, hatua ambayo itaendelea kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako