• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvutano baina ya Uholanzi na Uturuki kuongezeka endapo Waziri wa Uturuki kusimamishwa mjini Rotterdam

    (GMT+08:00) 2017-03-12 18:22:11

    Mvutano wa kidiplomasia kati ya Uholanzi na Uturuki uliibuka Jumamosi usiku baada ya msafara wa Waziri wa familia na Sera za kijamii wa Uturuki Betul Sayan Kaya kusimamishwa kwa masaa karibu na Ubalozi wa Uturuki mjini Rotterdam.

    Kaya alitaka kutembelea ubalozi wa Uturuki na kuzungumza katika mkutano wa hadhara juu ya kura ya maoni ya marekebisho ya katiba nchini Uturuki.

    Mapema jumamosi Serikali ya Uholanzi walizuia haki ya kutua kwa ndege ya Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Melvut Cavusoglu.

    Serikali ya Uturuki ilipanga kampeni nchini Uholanzi kama katika nchi nyingine za Ulaya kwa kuwataka wakazi wa Uholanzi wenye uraia wa Uturuki kupiga kura kwa ajili ya kumpa madaraka kubwa zaidi rais Recep Tayyid Erdogan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako