• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • La Liga: Ronaldo, Ramos waipaisha Madrid kileleni na mechi 1 mkononi

    (GMT+08:00) 2017-03-13 08:27:30

    Real Madrid usiku wa leo wametoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuiwasha Real Betis 2-1 Uwanjani Santiago Bernabeu Jijini Madrid nchini Hispania na kutwaa uongozi wa La Liga kutoka kwa Mahasimu wao Barcelona.

    Mapema usiku wa Jumapili, Barca walichapwa 2-1 na Deportivo La Coruna.

    Sasa Real wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 62 kwa Mechi 26 wakifuata Barca wenye Pointi 60 kwa Mechi 27.

    Real Betis, walifunga bao lao dakika ya 24 kwa Shuti dhaifu la Antonio Sanabria ambalo Kipa Keylor alidaivu na kulitema na Mpira kutiririka Wavuni.

    Real walisawazisha dakika ya 41 baada ya Krosi ya Marcelo kupigwa Kichwa na Cristiano Ronaldo na kutinga wavuni.

    Bao la ushindi la Real lilifungwa na Sergio Ramos katika Dakika ya 81 kwa Kichwa na kuwapa Real ushindi mtamu wa 2-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako