• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki watangaza hatua madhubuti dhidi ya Uholanzi

    (GMT+08:00) 2017-03-14 10:21:29

    Naibu waziri mkuu wa Uturuki Bw Numan Kurtulmus ametangaza kuwa Uturuki itachukua hatua za mfululizo dhidi ya Uholanzi, ili kujibu vitendo vyake vya kuwazuia maofisa wa Uturuki kuingia Uholanzi na kuwatawanya waandamanaji wa Uturuki nchini humo.

    Bw Kurtulmus amesema serikali ya Uturuki itasimamisha mazungumzo yote ya kisiasa na Uholanzi, ndege za wanadiplomasia wa Uholanzi hazitaruhusiwa kuingia Uturuki, na balozi wa Uholanzi nchini Uturuki ambaye sasa yuko nje pia haruhusiwi kuingia Uturuki.

    Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki jana iliitaka Uholanzi iombe radhi kutokana na kumzuia waziri wake wa sera za jamii na familia Bi. Sayan Kaya kwenda kwenye ubalozi wa Uturuki nchini humo, na kufanya uchunguzi kuhusu polisi wake kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji wa Uturuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako