• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani inatafuta uhusiano wa kiujenzi na unaoelekezwa na matokeo na China

    (GMT+08:00) 2017-03-14 17:08:18

    Kaimu msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Susan Thornton amesema Marekani inapenda kufanya majadiliano ya kiujenzi na China ili kuziwezesha pande hizo kutafuta na kutatua matatizo kati yao.

    Thornton amesema hayo kabla ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson nchini China. Amesema katika ziara hiyo, Tillerson atajadiliana na maofisa wa serikali ya China kuhusu changamoto mbalimbali na pia maeneo ya ushiriiano ambayo pande hizo zinatarajia kuyahimiza na kuyafanyia majadiliano ili kuendeleza zaidi.

    Kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Tillerson atawasili Beijing jumapili ijayo baada ya kumaliza ziara zake nchini Japan na Korea Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako