• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:mashirika na kampuni yatakiwa kuajiri wahasibu waliohitimu

    (GMT+08:00) 2017-03-14 18:57:50

    Mashirika na kampuni za biashara yameshauriwa na taasisi ya umma ya uhasibu kuajiri wahasibu waliohitimu na vyeti sahihi kisheria ili kukabiliana na ufisadi na wezi katika biashara zao.

    Mwenyekiti wa taasisi hiyo Protazio Begumisa amesema hatua hiyo itapunguza hata visa vya ukwepaji ushuru.

    Hii ni baada ya utafiti mpya wa mwaka 2017 kuhusu uhasibu wa mali za biashara kugunduliwa kwamba haujafikia viwango sahihi vya serikali.

    Kampuni nyingi zinashindwa kuelezea mapato yao na matumizi pamoja na faida sahihi kabla na baada ya malipo ya ushuru.

    Aidha wahasibu wanaohitimu wamekosa kupata ajira kutokana na visa vya ongezeko la wahasibu bandia wanaoitisha mishahara duni .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako