• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Feri ya mtongwe kufungua fursa mpya za biashara

    (GMT+08:00) 2017-03-14 18:57:50

    Msongamano wa watu na magari ulioshuhudiwa katika feri ya Likono utapungua kwa kiasi kidogo kufuatia kuregeshwa tena kwa huduma za feri ya mtongwe.

    Hii ni baada ya Rais Kenyatta kuzindua huduma za feri za Mtongwe zilizosimamishwa miaka mitano.

    Kurejelewa kwa huduma hizo ni afueni kwa wakazi wa Mtongwe kwani kutapunguza msongamano kwenye mapito makuu ya Likoni.

    Huduma za feri huko Mtongwe zilisimamishwa mwaka 2011 baada ya serikali kuondoa feri mbili zilizochakaa.

    Muundo msingi ulioharibika pia ulikuwa mojawapo wa sababu zilizoifanya serikali kuondoa huduma hizo za feri.

    . Kuondolewa kwa feri hizo kulisababisha msongamano kwenye kivuko cha Likoni huku wakazi wa Mtongwe wakilalamika kwamba tangu kuondolewa kwa huduma hizo thamani ya nyumba zao imeshuka.

    Rais Kenyatta anafanya ziara ya eneo la pwani tangu siku ya Jumamosi ambapo amezindua na kukagua miradi kadhaa ya maendeleo na biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako