• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Bei ya bidhaa muhimu yaathiri mfumko

    (GMT+08:00) 2017-03-14 18:57:50

    Bei ya bidhaa muhimu kama vile chakula nchini Tanzania zimeendelea kuathiri moja kwa moja mfumko wa nchi hiyo.

    Wiki hii kwa mujibu wa utafiti wa biashara ,mfumko wa bei wa Taifa kwa Machi umeongezeka hadi kufikia asilimia 1.0 kutoka asilimia 0.8 ilivyokuwa Januari mwaka huu.

    Aidha, kwa kipimo cha mwaka mfumuko huo kwa Februari umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 ilivyokuwa Januari mwaka huu.

    Kuongezeka kwa mfumuko huo wa bei kunatokana na kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula, ambayo imeongezeka hadi asilimia 9.3 kutoka asilimia 8.2 iliyokuwa mwezi januari mwaka huu.

    Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya mfumuko wa bei wa Februari, Kaimu Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja alisema, bidhaa za vyakula zilizochangia kuongeza kwa fahirisi za bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 4.0, mahindi kwa asilimia 12.2 na unga wa mahindi kwa asilimia 10 pamoja na bidhaa nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako