Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China, Li amesema Rais wa China Xi Jinping na mwenzake Rais wa Marekani Donald Trump walifanya mazungumzo kwa njia ya simu mara baada ya Trump kuingia madarakani, ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Li amebainisha kuwa Rais wa Marekani na Viongozi waandamizi kutoka katika utawala wake wamekubaliana kuwa Marekani itaendelea kufuata sera ya China moja.
Ameongeza kuwa sera hii imefanya msingi mzuri usiotetereka wa ushirikiano kati ya China na Marekani licha ya kubadilika kwa mazingira, na kusema kuwa msingi huu hautodhoofishwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |