Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema China inaendelea kuwa injini muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa dunia unaofufuka taratibu.
Bw. Li Keqiang amesema hayo akikutana na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa mkutano wa 5 wa Bunge la 12 la umma la China mapema leo. Bw. Li amesema kuwa pato la taifa la China limezidi dola trilioni 11 za kimarekani, na lengo la ukuaji wa asilimia 6.5 halimaanishi kuwa mchango wa China kwa uchumi wa dunia utapungua. Ameongeza kuwa kupungua kwa kasi ya ukuaji kutaiwezesha China kuweka kipaumbele katika kuongeza ubora na ufanisi wa uchumi wake.
Bw. Li Keqiang pia ameeleza imani yake juu ya utulivu wa kifedha nchini China, akiondoa uwekezano wa kutokea kwa hatari za kimfumo na kusema serikali ina machaguo mengi ya kisera kushughukia masuala ya kifedha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |